Somo kutoka Isaya linaonyesha furaha ya ajabu. Katikati ya jangwa, mahali ambapo vitu haviwezi kuwa na maisha ni magumu, Mungu huja na baraka; halafu jangwa linabadilika.
Kila mtu anaendapo jangwani anajisikia kiu. Jua kali hukausha ardhi ya jangwa.
Kama ardhi ya jangwa, mioyo yetu hupasuka kwenye joto la maisha. Roho zetu ni kavu. Jangwa la maisha ni wasiwasi, hali ya isiyo ya usalama, na woga wa vitu vingi.
Lakini tazameni mahali hapa, sehemu ya Dodoma. Tazameni maua ya miti sasa. Mvua inanyesha katika jangwa.
Sisi tunasalimana: “Kristo: Tumaini letu.” Tumaini letu ni Kristo. Tumaini letu ni mtu ambaye aliwaambia watu msalabani, “Naona kiu.” Halafu kiu cha Yesu Kristu kilikatwa na ufufuo.
Tumaini letu si kitu kidogo. Hata wakati ya Majilio msalaba upo. Lakini ufufuo upo pia! Neema za Mungu zipo! Kuna neema za Mungu tele duniani. Neema za Mungu zinanyesha, na kuna tumaini jangwani kwa maisha yetu mapya.
Bila shaka:
Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi,
jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi;
litachanua maua mengi,
na kufarahi, naam, kwa shangwe na kuimba.
Short, but sweet.
Translation? Try Google Translator.
No comments:
Post a Comment